Mwanachama wa DART WORKERS SACCOS ni mtu anayechangia akiba kila mwezi katika chama.

Chama Kinaundwa na:

Watumishi wa DART na mtumishi yoyote wa umma
Familia ya mtumishi wa DART ambao ni wenza na watoto
Wamiliki wa biashara ya usafirishaji Dar es Salaam

Je ni mtu yeyote anaweza kujiunga na DART SACCOS?

Hapana ila ni mtumishi wa DART, mtu yoyote aliyeajiriwa sekta ya utumishi wa umma, mtu yoyote anayetokana na familia ya mtumishi wa DART i.e wenza na watoto pamoja na mmiliki au kampuni ya biashara ya usafirishaji Dar es Salaam.

JINSI YA KUJIUNGA NA DART SACCOS

Kujaza fomu ya kujiunga inayopatikana ofisi za DART WORKERS SACCOS LTD au kwenye tovuti ya chama.

 1. 1. Kulipa ada ya kiingilio 200,000 na
 2. 2. Kulipa angalau hisa 10 @50,000

HUDUMA ZA KIFEDHA

Mwanachama anaruhusiwa kuweka Akiba (savings) au kulipa deni la DART WORKERS SACCOS LTD kupitia benki. Malipo yoyote yanayofanyika kwa mwanachama ni kwa njia ya Hundi au kwenye akaunti yake.

UKOMO WA UANACHAMA

Kuhamia sekta au makampuni binafsi isipokuwa sekta ya usafirishaji Kuacha/kufukuzwa kazi serikalini

MAADILI YA DART SACCOS

 1. 1. Kufanya kazi kwa ubunifu, bidii na maarifa
 2. 2. Uadilifu na uaminifu
 3. 3. Kuendeleza mifumo Chanya yenye tija kwa chama
 4. 4. Kutoa huduma bora yenye manufaa kwa wanachama
 5. 5. Umoja na ushirikiano
 6. 6. Uwazi na uwajibikaji
 7. 7. Kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii
 8. 8. Kupiga vita dhidi ya rushwa
 9. 9. Kuheshimu usawa wa kijinsia katika uongozi wa SACCOS