Kuuza hisa kwa wanachama

Mwanachama atatakiwa kununua hisa moja hadi kumi kila mwezi bila kukosa ili kutekeleza masharti ya kuwa mwanachama. Hisa moja inathamani ya shilingi elfu Hamsini. Mwanachama mpya atatakiwa kuingia na kiingilio cha shilingi laki mbili isiyorudishwa. Pia Mwanachama mpya atapaswa kununua idadi ya hisa kumi zenye thamani ya shilingi laki tano(500,000/=).

Kupokea akiba/amana za wanachama

Chama hupokea na kutunza hisa za hiari ambazo mwanachama amewekeza kwa ajili ya kukuza mtaji ambao unaweza kutumika kama dhamana ya mkopo au akiba. Mwanachama ataruhusiwa kuingiza kiasi chochote kama hisa za hiari kwenye akaunti ya chama.

Kutoa mikopo ya dharura

Kiwango cha juu cha mkopo ni shilingi 1,000,000 na inatozwa riba asilimia 2% kwa mwezi. Muda wa juu wa marejesho ni miezi sita. Mkopo huu unatolewa ndani ya masaa 24 baada ya kukamilisha taratibu za maombi.

Kutoa Mkopo hakuna makasiriko

Kiwango cha chini cha mkopo huu ni Tsh 200,000/= na cha juu ni shilingi 1,000,000 na mwanachama atatozwa riba ya 5% kwa mwezi. Mkopo huu hurejeshwa ndani ya mwezi mmoja na hutolewa ndani ya dakika 20 baada ya kukamilika taratibu zote za maombi.

Mkopo wa sikukuu

Kiwango cha juu cha mkopo huu ni shiling 500,000/= na utatozwa riba ya 0.83%. Muda wa juu wa kurejesha mkopo huu ni miezi mitatu. Hutolewa kwa sikukuu za Eid, Krismasi na Pasaka.

Kutoa mikopo ya kulipia ada kwa wanachama, mtoto au tegemezi yeyote anayemuhusu mwanachama

Kiwango cha juu cha mkopo huu ni shilingi milioni kumi na atatozwa riba ya 0.8, muda wa kurejesha mkopo ni miezi 24. Mwanachama atapaswa kuthibisha ni mkopo wa elimu na ataupata ndani ya masaa 24 mara baada ya kuthibitisha taratibu zote.

Mikopo ya biashara

Kiwango cha juu cha mkopo huu ni mara tatu (3) ya Akiba na mwanachama hutozwa riba ya 0.83%. Muda wa kurejesha ni miezi 12-24. Kiwango cha juu cha mkopo kwasasa ni shilingi 10,000,000. Hutolewa mwanzoni wa mwezi kuanzia tarehe 1-5 ya kila mwezi.

Mikopo ya Maendeleo

Kiwango cha juu cha mkopo huu ni mara tatu (3) ya Akiba na kutoza riba ya 0.83%. Muda wa kurejesha ni miezi 12-24. Kiwango cha juu cha mkopo kwasasa ni shilingi 10,000,000. Hutolewa mwanzoni wa mwezi kuanzia tarehe 1-5 ya kila mwezi.

Mikopo ya viwanja

Mkopo huu utategemea na taratibu zitakazowekwa na mkutano mkuu kwa wakati huo.

Kulipa riba akiba za wanachama

Chama hupokea na kutunza akiba za wanachama kupitia makato kwenye mshahara, au mwanachama anaweza kulipia bank kiasi chochote zaidi ya makato anayokatwa katika mshahara wake, aidha chama kinalipa 1% -5% ya akiba za mwanachama alizoweka kwa mwaka.

Kutoa gawio kwa wanachama baada ya kupitishwa na mkutano mkuu

Chama kitatoa gawio kwa wanachama baada ya kukubaliana kwenye mkutano mkuu.

Kutoa elimu ya ujasiriamali na uwekezaji kwa wanachama wake

Chama kina utaratibu wa kutoa elimu ya ujasiriamali na uwekezaji kwa wanachama wake mara tatu kwa mwaka.